Alama sita za kuukaribia ubingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 May 2022
Alama sita za kuukaribia ubingwa

Kabla ya kuikabili Simba katika mchezo wa nusu fainali kombe la FA, May 28 vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga watacheza mechi mbili muhimu za ligi

Yanga ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi na alama 60, ushindi katika michezo hiyo miwili utawafanya wafikishe alama 66 na pengine kuhitaji alama nyingine tano tu kutangaza ubingwa

Ijumaa ya wiki hii Yanga itaikaribisha Mbeya Kwanza katika mchezo utakaopigwa May 20 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Baada ya mchezo huo, Yanga itakwea pipa kuelekea jijini Mwanza ambako wanakabiliwa na mchezo dhidi ya Biashara United ambao utapigwa May 23 katika uwanja wa CCM Kirumba

Ni ratiba yenye changamoto lakini kwa hakika kama kocha Nasreddine Nabi na vijana wake watafanikiwa kushinda mechi hizi, watapiga hatua muhimu sana kuelekea ubingwa wa 28

Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema wameweka mkakati wa kuhakikisha wanapata matokeo katika michezo hiyo kwani hawahitaji kutegemea matokeo ya watani zao kuweza kushinda ubingwa

"Tuna nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa lakini hatupaswi kubweteka kwani bado kazi haijamalizika. Michezo hii inayofuata ina umuhimu mkubwa kwetu kupata alama zote sita. Tunahitaji kushinda mechi zetu kujihakikishia ubingwa pasipo kujali matokeo ya wapinzani wetu, " alisema Manara

Yanga inahitaji alama 11 tu katika michezo sita iliyobaki ili kujihakikishia ubingwa wa 28

Baada ya michezo ya nusu fainali kombe la FA, Ligi itasimama kwa takribani wiki tatu kupisha kalenda ya CAF mechi za timu za Taifa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2023

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’