FT : Yanga 4-0 Mbeya Kwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
20 May 2022
FT : Yanga 4-0 Mbeya Kwanza

Alama sita zimesalia kwa Yanga kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu baada ya leo kuichapa Mbeya Kwanza mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Yanga iliingia katika mchezo huo ikiwa na dhamira moja, kuzisaka alama tatu muhimu kuelekea ubingwa

Mbeya Kwanza waliingia katika mchezo huo kwa kujilinda zaidi lakini mbinu yao ilivurugwa na Yanga kwenye dakika ya 34, Fiston Mayele akifunga bao lake la 13 baada ya krosi murua kutoka kwa Salum Abubakar 'Sure Boy'

Kuingia kwa bao hilo kuliifanya Yanga iongezea mashambulizi langoni kwa Mbeya Kwanza na kufanikiwa kufunga mabao mengine mawili kabla ya mapumziko kupitia kwa Saido Ntibazonkiza na Dickson Ambundo

Yanga iliendelea kutawala mchezo katika kipindi cha pili ambapo kwenye dakika ya 60 kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alifanya mabadiliko kwa kuwaingiza wachezaji wanne Chrispine Ngushi, Chico Ushindi, Heritier Makambo na Zawadi Mauya

Makambo akafunga bao lake la kwanza msimu huu kwenye dakika ya 72 akiunganisha pasi ya kichwa kutoka kwa Ushindi

Ulikuwa mchezo ambao Yanga ingeweza kufunga mabao mengi zaidi kama wangetumia vyema nafasi nyingi walizotengeneza

Yanga sasa imefikisha alama 63 ikiongoza ligi kwa tofauti ya alama 13 dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili

Ushindi katika michezo miwili ijayo itatosha kuipa Yanga ubingwa

Aidha kama Simba itapoteza mchezo dhidi ya Geita Gold Jumapili, Yanga inaweza kutwaa ubingwa Jumatatu kama watapata ushindi dhidi ya Biashara United

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →