FT : Biashara United 1-1 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 May 2022
FT : Biashara United 1-1 Yanga

Mchezo wa ligi kuu kati ya Biashara United dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba umemalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Yanga ilitangulia kufunga bao kwenye dakika ya 74 kupitia kwa Fiston Mayele aliyeunganisha krosi murua ya Juma Shabani

Collins Opare akaisawazishia Biashara United dakika tatu baadae akitumia makosa ya wachezaji wa Yanga waliochelewa kuzuia shambulizi la kushitukiza

Hata hivyo ni mchezo ambao Yanga ingeweza kuumaliza tangu kipindi cha kwanza, Chico Ushindi, Dickson Ambundo na Mayele wakikosa nafasi muhimu

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi leo aliwapumzisha baadhi ya wachezaji, Yannick Bangala, Djigui Diarra, Khalid Aucho na Salum Abubakar 'Sure Boy' wote hawakuwa sehemu ya mchezo huo

Yanga imeongeza alama moja ikifikisha alama 64 sasa wakihitaji alama tatu katika michezo minne iliyobaki ili kustwaa ubingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
16h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’