Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema kikosi cha Yanga kiko tayari kuikabili Lipuli FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 16 kesho.
Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi kwenye dimba la Samora, mkoani Iringa.
Ten ambaye yuko Iringa amesema ari ya wachezaji wa Yanga iko juu baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi katika michezo mitatu iliyopita.
Licha ya kukiri mchezo huo wa ugenini unatarajiwa kuwa mgumu, Ten amesema Yanga imefuata alama tatu Iringa ili kuhakikisha inaweka hai matumaini ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo.
Yanga imetua Iringa ikitokea mkoani Mbeya ilikocheza mchezo wa kombe la FA hatua ya 32 bora dhidi ya Ihefu FC na kufanikiwa kuvuka raundi ya 16 bora baada ya ushindi wa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia matokeo ya sare ya bao 1-1.

ADVERTISE HERE