Kumbe Feisal aliwapania kwelikweli Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 May 2022
Kumbe Feisal aliwapania kwelikweli Simba

Kiungo wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto', aliyefunga bao pekee kwenye mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Simba, amefichua kuwa aliwasoma vizuri viungo wa Simba na kubaini madhaifu yao ambayo aliyatumia kuwaadhibu

Fei Toto alifunga bao hilo dakika ya 25 ya mchezo kwa shuti kali la mbali, amesema aliwafanyia mazoezi ya siku tatu viungo wa Simba, baada ya kugundua kuwa hawana kasi.

Fei Toto anayesifika kwa kupiga mashuti ya mbali, alisema kuwa hawakuwa na muda mrefu wa kujiandaa na mechi hiyo, lakini walitumia siku tatu kuisoma Simba, ndipo alipogundua udhaifu huo.

"Nilikuwa nawaangalia viungo wa Simba wanavyocheza, uzuri wao na udhaifu wao, kuna baadhi ya wachezaji wanaocheza eneo la kiungo hawana kasi, ni wachezaji wazuri, lakini wana udhaifu huo, hivyo nikatafuta ni jinsi gani ya kuutumia udhaifu huo"

"Siyo kila mchezaji amekamilika, hata mimi nina madhaifu yangu," alisema Feisal

Aidha kiungo huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' amesema siri ya kupiga mashuti ni mazoezi binafsi ambayo anayafanya, lakini pia uthubutu kwani siyo kila shambulizi ni lazima wachezaji wafike hadi kwa golikipa.

"Nimefunga mabao haya msimu huu kama matatu hivi, unajua kuna maeneo ukisogea unaona umjaribu kipa, golikipa naye ni binadamu, zingine zinakataa, zingine huwa zinakubali. Nilisogea nikaona sikabwi, na kuna nafasi ya kupiga, nikapiga"

Fei Toto amekuwa na kawaida ya kufunga mabao kwa mashuti makali msimu huu akifunga mabao ya aina hiyo pia katika michezo ya ligi kuu dhidi ya KMC na Ruvu Shooting

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’