Wachezaji wa Yanga kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, wamemshukuru mkongwe Saido Ntibazonkiza kwa nyakati nzuri alizoshiriki msimu huu
Saido alikuwa mchezaji mwenye ushirikiano wa karibu na wenzake, ambao walimuheshimu kutokana na uandamizi wake
Saido ndiye mchezaji aliyekuwa na mafanikio zaidi katika kikosi cha Yanga akicheza soka la kulipwa barani Ulaya kwa zaidi ya miaka 10 lakini pia aliwazidi wachezaji wote kwa umri
"Nina furaha nimekuwa na wakati mzuri nawe, nakutakia mafanikio mema na nakushukuru kwa kila kitu," aliandika Yacouba
"Sina maneno mengi ya kusema, lakini fahamu nakupenda, nakutakia mafanikio mema katika majukumu yako kaka," aliandika Aucho
"Nakutakia kila la kheri najua sio mwisho wetu kwa sababu ulikuwa unamchango mkubwa kwangu ntaendelea kukukumbuka ntakumiss sana najuwa tutaendelea kuwasiliana lakini bado ulikuwa unaumuimu kwangu nakupenda kaka yangu," aliandika mshambuliaji Fiston Mayele
Ukweli ni kuwa wengi wamegushwa baada ya Yanga kutangaza kuachana na mkongwe huyo baada ya mkataba wake kumalizika
Msimu huu Saido alikuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Yanga akifunga mabao saba na kutoa pasi tano za mabao katika mashindano yote
Licha ya kuwa hatashiriki katika michezo iliyobaki, Saido ataingia katika kumbukumbu kuwa mmoja wa wachezaji waliochangia ubingwa wa Yanga msimu huu
Imeelezwa kuwa Yanga imechukua uamuzi huo baada ya kushindwa kufikia nae makubaliano katika mkataba mpya
Yanga ilikuwa tayari kumpa mkataba wa mwaka mmoja lakini yeye alihitaji mkataba wa miaka miwili