Kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajib anatarajiwa kukosa mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Lipuli FC imefahamika.
Ajib alipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Azam FC na hakuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichoivaa Ihefu FC katikati ya wiki.
Huo unakuwa mchezo wa pili kwa Ajib kukosa kwenye ligi, alikosa mchezo dhidi ya Mbao FC akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
Pamoja na Ajib, Haji Mwinyi, Abdallah Shaibu na Pato Ngonyani nao wataukosa mchezo huo kutokana na majeruhi.
Thabani Kamusoko na Donald Ngoma bado hawako fiti licha ya kuelezwa kwamba wamepona majeraha yao.
Yanga itashuka kwenye dimba la Samora kesho ikiwa na lengo moja tu la kuibuka na ushindi ili kuweka hai matumaini ya kutetea ubingwa wake.

ADVERTISE HERE