Klabu ya Yanga imetangaza tarehe ya kufanyika Uchaguzi Mkuu wa kuwapata viongozi wapya wa klabu hiyo
Aidha Yanga imeagiza Matawi yote yaliyokidhi vigezo kuhakikisha wanakamilisha chaguzi zao za ndani na kuwasilisha majina ya viongozi waliochaguliwa kwa Mtendaji Mkuu wa klabu
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Malangwe Mchungahela amesema viongozi wa Matawi ambao watachaguliwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Mzaidizi, Mweka Hazina na Wajumbe wasiozidi watano (wawili watashiriki Mkutano Mkuu)
Uchaguzi Mkuu wa viongozi wa juu wa klabu utahusisha Rais, Makamu wa Rais na Wajumbe Watano
Uchaguzi utafanyika Julai 10 2022 ambapo mchakato wa uchaguzi huo umeanza rasmi leo baada ya kutangazwa
Fomu zitaanza kutolewa Juni 5 hadi Juni 9 ambapo kikao cha mchujo wa awali kitaketi Juni 10-11
Mapingazi yatapokelewa Juni 13-15 na kupitiwa Juni 16-18 ambapo majina ya wagombea waliopitishwa yatatangazwa Juni 19-20
Pia kutakuwa na muda wa kukataa rufaa kwa wagombea walioenguliwa kabla ya kuanza kwa kampeni Julai 5 mpaka Julai 09
Gharama ya kuchukua fomu kwa anayegombea nafasi ya RAIS wa klabu na MAKAMU wa Rais ni Tsh laki (2) kila mmoja wakati upande wa nafasi ya Wajumbe ni Tsh laki (1)