Baada ya kufanikiwa kupata alama moja kule Benin kwa kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Niger, timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imerejea nchini kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Algeria
Tanzania itakuwa mwenyeji wa Algeria siku ya Jumatano, Juni 08 katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mkakati wa kikosi cha Kim Poulsen ni kuhakikisha ushindi unapatikana katika michezo yote mitatu itakayopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Algeria ndio vinara wa kundi F wakiwa na alama tatu baada ya kuichapa Uganda mabao 2-0 hapo jana
Niger na Tanzania zinafuatia kila moja ikiwa na alama moja wakati Uganda inaburuza mkia
Wakati Tanzania ikichuana na Algeria siku ya Jumatano, Uganda itachuana na Niger
ADVERTISE HERE