Jana katika mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2023 kati ya Niger dhidi ya Tanzania, kocha Mkuu wa Stars Kim Poulsen alilazimika kufanya mabadiliko ya mapema kwenye safu ya ulinzi upande wa kulia akimtoa Haji Mnoga nyota anayecheza kule Uingereza na kumuingiza Kibwana Shomari
Mnoga alikuwa na wakati mgumu kumdhibiti winga hatari wa Niger Victorien Adebayor ambaye jina lake sio geni sana hapa Tanzania
Adebayor ndiye aliyekuwa mfungaji bora wa michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika akiitumikia USGN ya huko Niger
Baada ya kuingia Kibwana mambo yalibadilika, Adebayor hakuonekana tena uwanjani, Kibwana alifanikiwa kuziba njia zote akishirikiana na Dickson Job ambaye pia alionyesha kiwango bora katika mchezo huo
Hatimaye kinara huyo wa kupachika mabao katika kikosi cha Niger alitolewa kwenye kipindi cha pili akimuacha Kibwana anapanda na kushuka upande wa kulia
Huyu ndiye Kibwana ambaye Wananchi wanamfahamu! Hajawahi kushindwa pale anapokabidhiwa kazi maalum!