Nahitaji kupumzika - Mwambusi

Admin By Admin
β€’
13 Jul 2017
Nahitaji kupumzika - Mwambusi
Aliyekuwa kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema amejipa likizo ya kufundisha soka kwa angalau msimu mmoja ili ajikite katika mambo yake binafsi.

Mwambusi aliyeitumikia Yanga kwa misimu miwili mkataba wake umemalizika Juni 30, ameiaga rasmi klabu yake hiyo aliyotwaa mataji ya VPL kwa misimu yote aliyokuwa nayo.

"Mkataba wangu na Yanga SC umemalizika toka June 30, Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa misimu yote miwili na tumeweza kushirikiana Uongozi wachezaji , mashabiki na wapenzi pamoja na wanachama kuhakikisha Yanga yetu inapata mafanikio," amesema Mwambusi.

"Sitokuwa kwenye mpira kidogo kwa hiyo watanikosa wadau soka, Nitakuwa katika mambo binafsi kwa msimu wote nahitaji kupumzika, kwa hiyo nadhani msimu utakaokuja mwingine inshaallah Mwenyezi Mungu akitupa uhai tutaungana tena katika gurudumu hili la kulisogeza soka letu mbele"

Baada ya kuondoka Yanga Mwambusi alikuwa anahusishwa kuungana na kocha wa zamani wa Yanga Hans van Pluijm anayeinoa Singida United.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’