Yanga inanukia 'fedhwa'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jun 2022
Yanga inanukia 'fedhwa'

Kiasi kikubwa cha fedha ambacho Yanga itakivuna mwishoni mwa msimu kinaipa jeuri ya kunasa mastaa katika timu yoyote barani Afrika na ikamudu kuwalipa mishahara na posho bila presha kwa mkataba wa miaka miwili.

Ikiwa itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu, Yanga itajihakikishia kitita kisichopungua Sh 4 bilioni ambacho kinatokana na mikataba minono ambayo imesaini na kampuni tofauti lakini fedha za zawadi kwa washindi wa Ligi.

Kiasi kikubwa cha fedha itavuna kupitia mkataba wake wa maudhui na kampuni ya Azam Media ambao kuna kipengele kinachoipa fursa ya kupata kitita cha Sh 3 bilioni kama bonasi kwa kutwaa ubingwa au kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi kila msimu.

Timu hiyo itapata pia kiasi cha Sh 500 milioni kutoka Azam Media kama fedha za bonasi au zawadi kwa bingwa wa Ligi Kuu ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya mkataba wa haki za matangazo ya ligi baina ya kampuni hiyo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Yanga pia inaripotiwa itapata bonasi ya Sh 500 milioni kutoka kwa wadhamini wao wengine, kampuni ya GSM ikiwa watatwaa ubingwa wa ligi pia watapewa kiasi cha Sh 100 milioni na mdhamini wao mkuu, kampuni ya Sportpesa.

Jana uongozi wa Yanga ulitangaza kukusanya takribani Tsh Bilioni 1.07 kutokana na usajili wa Wanachama ambapo fedha hizo zitaiongezea Yanga jeuri pale itakapokwenda sokoni kuwasaka nyota watakaojiunga na timu hiyo kwa ajili ya kuimarisha kikosi kuelekea msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
2h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
14h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’