Mambo muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jun 2022
Mambo muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu Yanga

Ikiwa zoezi la kuchukua fomu limefungwa rasmi, ni vyema Wananachama wa Yanga mkafaham masuala yafuatayo;

1. Klabu ya Yanga inaongozwa kwa Mujibu ya Katiba yake ya 2021 na kanuni zake, Katiba ya TFF na kanuni zake, Katiba ya CAF na kanuni zake, Katiba ya FIFA na kanuni zake pamoja na Sheria za nchi.

2. Sifa kuu ya kuwa na Kiongozi wa Yanga ni lazima uwe Mwanachama hai, una umri kuanzia 25-75, uwe raia wa Tanzania, uwe mwanachama kwa kipindi kisichopungua miaka 4, na uwe na elimu inayohitajika kutokana na nafasi unayogombea na usiwe umewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai basi, nje na hapo hakuna kinachomzuia mwanachama kugombea nafasi ya Uongozi.

3. Mkutano maalum wa uchaguzi Matawi yatawakilishwa na wajumbe wa 5 tu kila tawi, kwa maana ya Mwenyekiti, Katibu, Mwekahazina, na wajumbe wawili wa mkutano mkuu ngazi ya tawi, hivyo kama kuna tawi halina wanachama kuanzia 100 na halijafanya uchaguzi halitakuwa na haki ya kuudhulia mkutano wa uchaguzi (Klabu itatumia database yake kuhakiki hili jambo).

4. Uchaguzi wa Rais na Makamu utaamuliwa na wingi wa kura 51% za wajumbe walioudhuria na wenye haki ya kupiga kura huku Uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji utaamuliwa na wagombea 5 wa kwanza walioongoza kwa wingi wa kura zilizopigwa.

5. Endapo kuna wagombea zaidi ya mmoja ambao kura zao zimelingana, basi wagombea hao watashindana kwenye duru ya pili.

Imeandikwa na Simon Patrick, Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama, Yanga Sc

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’