Uongozi wa Yanga umethiitisha kuwa mlinda lango namba moja, Youthe Rostand hatakuwemo kwenye kikosi cha Yanga kitakachoivaa Njombe Mji keshokutwa Jumanne, Debruari 06.
Rostand aliumia kwenye mchezo dhidi ya Lipuli FC na alilazimika kubaki Iringa kwa matibabu zaidi asubuhi kabla ya kurejea Dar es Salaam jioni ya leo kwa usafiri wa ndege.
Wakati huo huo mlinda lango Benno Kakolanya amerejea kikosini baada ya kupona majeraha yake.
Kakolanya pamoja na Ramadhani Kabwili ndio wanaotegemewa kuibeba Yanga kwenye mchezo dhidi ya Njombe Mji pengine na ule wa ligi ya mabingwa dhidi ya St Louis Jumamosi ijayo.

ADVERTISE HERE