Michezo ya mzunguuko wa 16 ligi kuu ya Vodacom imekamilika leo kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Mbao FC kuilaza Kagera Sugar mabao 2-1 na Stand United kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1.
Hakuna mabadiliko kwenye nafasi nne za juu kwa kuwa Simba, Azam FC, Yanga na Singida United zote zimeshinda michezo yao ya mzunguuko wa 16.
Mzunguuko wa 17 unatarajiwa kuendelea keshokutwa Jumanne kwa Yanga kushuka katika uwanja wa Taifa kuivaa Njombe Mji wakati Simba na Azam FC zitaumana Jumatano.
Bado ligi ni mbichi. Licha ya Simba kuongoza kwa tofauti ya alama tano, bado ni mapema sana kwa mashabiki wake kushangilia ubingwa.
Bado kuna michezo 14 sawa na alama 42 za kuwaniwa. Jambo pekee la kufurahiwa na mashabiki wa vinara hao wa ligi sasa ni kuongoza ligi pamoja na idadi kubwa ya mabao wanayofunga kwenye michezo yao.

ADVERTISE HERE