Da! wachezaji 11 kuikosa Njombe Mji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Feb 2018
Da! wachezaji 11 kuikosa Njombe Mji
Yanga inashuka dimbani kesho Jumanne kuivaa Njombe Mji kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 17.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Taifa kama hakutakuwa na mabadiliko ya uwanja.

Daktari wa Yanga Dk Edward Bavu amethibitisha wachezaji 11 majeruhi hawatakuwemo kwenye mchezo huo.

Hawa 11 wanaunda kikosi cha majeruhi! Kikosi ambacho kama wote wangekuwa timilifu wangeweza kushusha dozi ya maana pale uwanja wa Taifa.

1.YOUTHE ROSTAND
2.JUMA ABDUL
3.HAJI MWINYI
4.ABDALLAH SHAIBU
5.ANDREW VICENT
6.PATO NGONYANI
7.YOHANA NKOMOLA
8.THABAN KAMUSOKO
9.AMISSI TAMBWE
10.DONALD NGOMA
11.IBRAHIM AJIB

Hata hivyo kukosekana kwa wachezaji hao haiwezi kuwa sababu ya Yanga kukosa ushindi kesho.

Juzi tulishuhudia Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lipuli bila ya uwepo wa wachezaji hao.

Hii inadhihirisha kazi kubwa iliyofanywa na benchi la ufundi ya kutengeneza kikosi imara.

Naamini kwenye ligi msimu huu Yanga ndiyo timue yenye kikosi imara zaidi kwani imeweza kucheza michezo mingi bila ya kuwa na wachezaji wake muhimu.

Nina uhakika, sio Simba, Azam FC wala Singida United inayoweza kushuka dimbani bila ya kuwa na 'first eleven' halafu ikafanya vizuri kama ilivyo Yanga ya sasa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’