Uongozi kuchunguza majeruhi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Feb 2018
Uongozi kuchunguza majeruhi Yanga
Uongozi wa Yanga umeamua kulivalia njuga janga la majeruhi katika kikosi chake msimu huu.

Tangu kuanza kwa msimu, Yanga imekuwa ikiwakosa wachezaji wake waandamizi kwa nyakati tofauti kutokana na kuwa majeruhi.

Lakini sasa hali imezidi kuwa mbaya kutokana na kuwa na idadi kubwa ya majeruhi (wachezaji 11) kiasi cha kutishia kuathiri malengo ya timu hiyo msimu huu.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya utendaji amedokeza kuwa Yanga imeanza kuchunguza sababu hasa ya majeruhi ya mara kwa mara ya baadhi ya wachezaji na itachukua hatua kukabiliana na tatizo hilo.

Aidha Mjumbe huyo amedokeza kuwa wamemuagiza daktari wa timu kuchunguza afya ya mshambuliaji Donald Ngoma kujiridhisha na madai yake ya kuwa bado hayuko timilifu.

Yanga imedhamiria kuvunja mkataba wa mchezaji huyo kama itabainika amekuwa akiuhadaa uongozi. Ngoma amekuwa na safari za mara kwa mara kurudi kwao Zimbabwe kwenda kutibiwa.

Ukimuondoa Ngoma, wachezaji wengine ambao ni majeruhi wamekuwa wakitibiwa chini ya uangalizi wa daktari wa Yanga, Dk Edward Bavu.

Yanga imekumbwa na idadi kubwa ya wachezaji majeruhi kipindi ambacho inakabiliwa na michuano mingi.

Kama wachezaji hao hawataweza kurejea dimbani kwa wakati, Yanga inaweza kujikuta inapoteza wachezaji wengi zaidi kutokana na majeruhi.

Uhaba wa wachezaji utapelekea kikosi hichohicho kutumika kwenye ligi, kombe la FA na michuano ya ligi ya mabingwa.

Na kama itakuwa hivyo, itakuwa muujiza kwa Yanga kufanikiwa kutetea taji lake la ligi kuu na pengine hata kutwaa kombe la FA achilia mbali kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’