Mgombea pekee nafasi ya Urais wa Yanga Injinia Hersi Said amethibitisha kuwa wamekamilisha usajili wa wachezaji watano wa kigeni, wawili wakiwa tayari wametambulishwa ambao ni Lazarus Kambole na Bernard Morrison
Hersi ametamba kuwa katika wachezaji watatu wanaosubiri kutambulishwa, mmoja ni mcheza mwenye profile kubwa sana kuliko mchezaji yeyote hapa Tanzania
Mchezaji huo sio mwingine bali ni nyota wa Kimataifa wa Burundi, Gael Bigirimana
Ni kiungo ambaye ukihesabu timu alizocheza Ulaya inashtua kidogo lakini ni wazi Yanga imefanikiwa kumnasa Injinia Hersi akitamba ni usajili wenye thamani kubwa.
Gael amepitia klabu kama Coventry City, Newcastle United, Rangers na sasa Glentoran ya Ireland ya Kaskazini.
GSM imefanya ushawishi mkubwa kuweza kumrejesha Afrika. Lakini hii sio mara ya kwanza kwa Yanga kwani pia waliweza kumshawishi Saido Ntibazonkiza kuja Tanzania kuwatumika Wananchi
Bigirimana ambaye ni tegemeo kwenye timu ya Taifa ya Burundi amewahi kutamba na Newcastle United ya England. Ni aina ya kiungo mnyumbulifu ambaye anaweza kucheza eneo lote la kati, mchezaji wenye mapafu ya mbwa