FT : Yanga 4-0 Njombe Mji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Feb 2018
FT : Yanga 4-0 Njombe Mji
Licha ya kukabiliwa na majeruhi wengi, kikosi cha Yanga kimedhihirisha kuwa kiko imara kuliko wengi wanavyofikiria baada ya kuirarua Njombe Mji mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 17.

Mchezo huo umepigwa leo Jumanne kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Licha ya kutengeneza nafasi kadhaa kwenye kipindi cha kwanza, Yanga ilishindwa kuipenya ngome ya Njombe Mji hivyo kupelekea timu hizo kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana.

Kipindi cha pili ndio zahma ya mabao iliikumba Njombe Mji kwani kwenye dakika ya 46 Obrey Chirwa aliifungia Yanga bao la kuongoza kwa kuunganisha vyema krosi ya Pius Buswita.



Chirwa na Buswita wamekuwa na maelewano mazuri katika michezo ya hivi karibuni kwani wamekuwa wakitengenezeana mabao.

Kwenye dakika ya 54 mlinda lango wa Njombe Mji Mbululu alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuudaka mpira aliorudishiwa na mlinzi wake akiwa nje ya eneo lake.

Yanga sasa ikiwa na faida ya mchezaji mmoja zaidi iliendelea kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa Njombe Mji na ikaongeza bao la pili kwenye dakika ya 65 kupitia mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Njombe Mji kuuzuia kwa mkono mpira wa Chirwa uliokuwa unaelekea kimiani.

Ni Chirwa aliyefunga mkwaju huo, hilo likiwa bao lake la pili katika mchezo huo.

Yanga iliendelea kutawala mchezo huo na iliwachukua dakika nne kuongeza bao la tatu kwenye dakika ya 69 kupitia kwa Emanuel Martin aliyewahi mpira wa Juma Mahadhi ambao uligonga mwamba.

Mahadhi aliyeingia kuchukua nafasi ya Raphael Daudi aliichangamsha safu ya ushambuliaji.

Akiteleza kutoka winga ya kulia alipiga shuti lililogonga mtambaa panya kabla Martin hajawahi mpira huo na kuujaza kimiani kufunga bao lake la tatu msimu huu huku likiwa la tatu kwa Yanga leo.

Kuingia kwa mabao hayo kuliwafanya Njombe Mji wapoteane na kucheza kwa muda mwingi bila ya malengo.

Chirwa akaifungia Yanga bao la nne kwenye dakika ya 87 akiunganisha pasi murua ya Baruani Akilimali 'Kiberenge' aliyeingia kuchukua nafasi ya Emanuel Martini.

Chirwa amefunga hat-trik yake ya pili msimu huu sasa akiwa nyuma ya Emanuel Okwi kwa tofauti ya mabao mawili tu.

Baada ya mchezo huo Yanga sasa inahamishia nguzu zake kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ambapo Jumamosi, Februari 10 itawakaribisha Washelisheli, St Louis kwenye dimba la Taifa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’