Mayele anawasubiri Ngao ya Jamii

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jul 2022
Mayele anawasubiri Ngao ya Jamii

Kuna watu walishangilia zilipoibuka tetesi kuwa mshambuliaji Fiston Mayele atajiunga na klabu ya Kaizer Chiefs

Hata hivyo Yanga imeweka bayana kuwa haina mpango wa kumuuza Mayele ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Wananchi

Unajua kwa nini walifurahi baada ya kusikia Mayele anaondoka?

Msimu uliomalizika Yanga ilianza kuhesabu taji la kwanza kwenye Ngao ya Jamii, wakiwachapa Simba bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Ulikuwa mchezo wa kwanza kabisa kwa Mayele kujitambulisha rasmi kwenye soka la Tanzania

Baadae ikawa historia kwake kwani alijijengea umaarufu wa aina yake akimaliza msimu akifunga mabao 16 kwenye ligi pia akitoa pasi tano za mabao

Msimu huu tena utaanza kama ilivyokuwa msimu uliopita, mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa August 13

Mayele amepania kun'gara katika mchezo huo kama alivyofanya msimu uliopita

Nyota huyo kutoka DR Congo amesema wakati huu watachuana na Simba wakiwa imara zaidi kwani watapata muda wa kutosha kufanya maandalizi

"Tunatarajia kuwa na mchezo mgumu na wa ushindani mkubwa dhidi ya Simba, ila ukweli naamini safari hii tutawashangaza zaidi"

"Timu inatakiwa kujiandaa vyema ili kupata kile tunachostahili. Nakumbuka msimu ulioisha kwenye Ngao ya Jamii nilichezeshwa nikiwa sijafanya maandalizi ya kutosha kutokana na kubaki Morocco kwa janga la Uviko-19, ila wakati huu nitakuwa fiti sababu tuna muda wa kutosha kujiandaa," alisema Mayele

Wachezaji wa Yanga wanaingia kambini leo Avic Town ambapo siku ya kesho wataanza rasmi maandalizi ya msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’