Wazee Yanga wacharuka Manara kufungiwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jul 2022
Wazee Yanga wacharuka Manara kufungiwa

Wazee wa klabu ya Yanga wamewaagiza viongozi wa Matawi kukutana kwa dharura ili kutoa maazimio ya hatua za kuchukua kufuatia kufungiwa kwa msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara

Mkutano huo wa viongozi wa Matawi utafanyika leo Jumamosi, Makao Makuu ya klabu Jangwani jijini Dar es salaam

Wakizungumza na Wanahabari mapema leo, Wazee walieleza kusikitishwa na hatua iliyochukuliwa na Kamati ya Maadili kumfungia Manara miaka miwili pamoja na faini ya Tsh Milioni 20

"Tunaamini katika hukumu hii kuna shinikizo la Waziri wa Michezo (Mh. Mohammed Mchengelwa) kwani siku ya kutolewa tuzo za ligi kuu aliagiza Manara achukuliwe hatua kali jambo ambalo sisi tunaona sio sahihi"

"Lakini pia Manara alizozana na Rais wa TFF Karia, ila tunashangaa aliyeitwa mbele ya Kamati na kuchukuliwa hatua ni mtu mmoja tu?," alihoji Mzee Mohammed Msumi

Wazee wanaamini adhabu iliyotolewa ni kubwa na wanadhani busara ingeweza kutumika kumaliza shauri hilo

"Walifungiwa akina Mwakalebela lakini baadae Serikali ikaingilia kati na busara ikatumika kumaliza shauri lile. Kwa nini busara hiyo haikutumika kumaliza shauri hili la Manara ambalo sisi tunaona ni watu wawili ambao walizozana kutokana na presha ya mchezo kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union?," alisema Mzee Msumi

Wazee wamesema wataomba kwenda kuonana na Rais wa nchi Mh Mama Samia Suluhu Hassan kama jambo hili halitapatiwa mwafaka haraka

Wazee wanaamini Manara amefungiwa kimkakati ili kuivuruga Yanga kuelekea Tamasha la Wiki ya Mwananchi

"Kuna kesi nyingi mbele ya kamati ya Maadili mpaka leo hazijatolewa hukumu lakini hii ya Manara hukumu yake imetolewa haraka"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
18h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’