Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Ivory Coast kwa msimu wa 2021/22
Aziz Ki amemshinda tuzo hiyo akiwa na klabu ya Asec Mimosas akimshinda mshambuliaji Karim Konate aliyekuwa naye katika klabu ya Asec Mimosas
Konate alikuwa mfungaji bora katika ligi ya Ivory Coast
Ulikuwa msimu wa mafanikio kwa Aziz Ki akiwa na Asec Mimosas, Wananchi wana matumaini makubwa kuwa atarejea kile alichokifanya Ivory Coast akiwa na Yanga hapa Tanzania
Yanga ina wachezaji wawili walioshinda tuzo za wachezaji bora wa ligi katika msimu, Yannick Bangala aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora ligi kuu ya Tanzania na Aziz Ki

ADVERTISE HERE