Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe amesema michuano ya CAF Super Cup inayotarajiwa kuanzishwa barani Afrika itazinufaisha klabu zote zitakazoshiriki
Akizungumza katika Mkutano wa mwaka wa CAF unaofanyika jijini Arusha, Motsepe amesema wanafahamu changamoto kubwa inayokwamisha maendeleo ya soka la Afrika ni fedha pamoja na kuwa pia kuna changamoto ya viwanja
Amesema kupitia mashindano ya CAF Super Cup klabu zitapata fedha nyingi
"Ukiacha viwanja tatizo kubwa kwa mpira wa Afrika ni fedha. Nimshukuru Rais wa FIFA Gianni Infantino kwa kutupatia wazo hili"
"Kupitia mashindano haya mapya ya CAF SUPER LEAGUE klabu zitapata fedha nyingi ambapo kwanza kila klabu itapata dola milioni 2.5 kwa ajili ya kusajili wachezaji na gharama za michuano kama usafiri na hotel lakini pia bingwa atapata dola za Marekani Milion 100," alisema