Wasifu wa St Louis inayochuana na Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Feb 2018
Wasifu wa St Louis inayochuana na Yanga
St Louis inashiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu huu ikiwa mabingwa wa soka wa Ushelisheli pia ikiwa ni mabingwa wa kombe la shirikisho nchini humo.

Imetwaa mataji mawili kwa mara ya kwanza msimu uliopita.

Timu hiyo inayotoka wilaya ya St Louis ilijihakikishia ubingwa wa ligi mapema tu na ilifanikiwa kuichapa Anse Reunion kwa mabao 3-1 kwenye mchezo wa fainali kombe la shirikisho (FA yao).

Mara ya mwisho St Louis kutwaa ubingwa wa Shelisheli ilikuwa mwaka 1994 hivyo imesubiri kwa miaka 23 kabla ya kutwaa ubingwa tena.

Timu hiyo ilipata mafanikio msimu uliopita wakati ikinolewa na kocha ambaye hakuwa na leseni inayotambuliwa na CAF, Nigel Freminot.

Ililazimika kuachana na kocha huyo kutimiza mahitaji ya sheria za CAF ili iweze kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa.

Kocha wake wa sasa Michel Renald hana hata mwezi mmoja tangu akabidhiwe kibarua ya kuinoa timu hiyo.

Msimu uliopita timu kutoka Ushelisheli ambayo ilishiriki ligi ya mabingwa inaitwa Cote d'Or ilitolewa kwenye hatua ya awali na St George ya Ethiopia kwa kuchapwa jumla ya mabao 5-0.

Japo mpira unadunda, lakini Yanga ikikomaa ina nafasi nzuri ya kusonga mbele hatua inayofuata katika michuano ya ligi ya mabingwa.

Muhimu ni kuhakikisha inapata ushindi mnono kwenye mchezo unaopigwa uwanja wa Taifa kesho.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’