Nabi awapa nyota wapya miezi miwili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Aug 2022
Nabi awapa nyota wapya miezi miwili

Licha ya kucheza mechi mbili za kimashindano, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema kwa sasa ni mapema kutoa tathimini ya ubora wa wachezaji wake wapya na badala yake anawapa muda wa miezi miwili hadi mitatu.

Wachezaji wapya wa Yanga ambao imewasajili msimu huu ni Stepnane Aziz Ki raia wa Burkina Faso, Mrundi Gaël Bigirimana, Mghana Bernard Morrison, Joyce Lomalisa (DR Congo) na Lazarous Kambole raia wa Zambia ambaye hata hivyo hajaonekana uwanjani akisumbuliwa na majeraha

Mchezo wa kwanza wa mashindano, Yanga iliibuka na ushindi mabao mawili dhidi ya Simba kwenye Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi iliyopita kabla ya juzi kupata matokeo kama hayo dhidi ya Polisi Tanzani katika mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu msimu huu iliyopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha

Nabi amebainisha kuwa kutopata maandalizi mazuri ya msimu mpya (Pre-Season), hawezi kutoa tathmini ya wachezaji wake wapya na anawapongeza nyota wake kwa kupambana kutafuta matokeo.

"Kwa sasa ni mapema kutoa tathmini za wachezaji wangu wapya na nimewapa muda wa miezi miwili hadi mitatu baada ya hapo ndiyo naweza kutoa tathimini kwa sababu watakuwa wameshazoeana na kutengeneza muunganiko mzuri na wachezaji waliowakuta," alisema Nabi.

Kikosi cha Yanga kimeendelea kubaki mkoani Arusha ambapo kesho Jumamosi, watashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuumana na Coastal Union katika mchezo wa pili wa ligi kuu msimu huu

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’