Msemaji na Mhamasishaji wa Yanga Haji Manara leo ametimiza mwaka mmoja tangu alipojiunga na mabingwa hao wa kihistoria Tanzania
Wakati Manara anajiunga na Yanga akitokea klabu ya Simba wapo ambao hawakuwa na imani kama atafanya kazi vyema wengi wakikumbuka mashambulizi aliyokuwa akiyarusha Yanga
Hata hivyo tunaweza kusema mwaka wake mmoja na Yanga umekuwa na mafanikio makubwa
Manara amekuwa sehemu ya uongozi ambao umefanikisha Yanga kushinda mataji yote katika msimu uliopita
Katika matukio makubwa ambayo yameacha alama Manara akiwa ameshiriki kikamilifu ni shamrashamra za ubingwa wa ligi kuu ambazo ziliitikisa Afrika
Manara ameshiriki katika maandalizi ya kila hatua ya tukio lile ambalo kwa kiasi kikubwa limechangia kuitangaza Yanga barani Afrika na hata nje
Kocha maarufu Pitso Mosimane, kocha wa zamani wa Mamelod Sundowns na Al Ahly kuja kushiriki kilele cha wiki ya Mwananchi, mwanzo ni zile shamrashamra za ubingwa
Mosimane alieleza kuvutiwa na tukio lile akibainisha kuwa Yanga imezifundisha klabu za soka Afrika kuwa nao wanaweza kushangilia ubingwa kama wafanyavyo watu wa Ulaya
Kwa sasa hakuna anayeweza kuwa na mashaka na 'Uwananchi' wa Manara. Sasa anatumikia kifungo cha TFF kwa sababu amekuwa akiipigania Yanga
Sisi Wananchi tunampa moyo aendelee kuipambania Yanga, tunamuunga mkono...!