Katika mwezi huu Septemba 2022, Yanga itacheza mechi tano. Ligi Kuu ya NBC kutakuwa na mechi tatu na mbili ni katika michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya awali
Septemba 06 Wananchi watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Azam Fc kabla kuelekea Chamazi kuwakabili Zalan Fc katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya awali, Septemba 10
Siku tatu baadae Wananchi watashuka tena dimba la Mkapa kuwakabili Mtibwa Sugar kabla ya kurejea tena kwa Mkapa kuikabili Zalan Fc katika mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa Septemba 17
Mchezo mwingine utapigwa Septemba 29 dhidi ya Ihefu Fc mkoani Mbeya

ADVERTISE HERE