Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' jioni ya leo watashuka dimbani huko Uganda kuumana na wenyeji wao Uganda Cranes katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya CHAN 2023 ambayo itafanyika nchini Algeria
Tanzania inahitaji kushinda mchezo huo kwa angalau mabao mawili baada ya kupoteza mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kwa bao 1-0
Kocha Mkuu wa Stars Honor Janza amesema licha ya kupoteza mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam, wana nafasi ya kupata ushindi huko Uganda
"Tumefanya maandalizi muhimu na tumekuja hapa Uganda kutafuta ushindi. Hakuna jambo lisilowezekana kama wao walishinda kwetu basi na sisi tunaweza kuwafunga hapa kwao," alisema
ADVERTISE HERE