Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema ushindi wa bao 1-0 iliyopata Yanga dhidi ya St Louis sio matokeo mabaya japo hayajawaridhisha wengi.
Akizungumza baada ya mchezo Nsajigwa amesema mfumo wa kupaki basi uliotumiwa na wapinzani wao umechangia kwa kiasi kikubwa Yanga kupata ushindi huo kiduchu.
Hata hivyo amesema wana matumaini ya kufanya vizuri zaidi kwenye mchezo wa marudiano kwa kuwa wapinzani wao hawatapaki basi.
"Wao walikuja na mbinu ya kucheza watu tisa nyuma ya mpira. Tulijaribu kubadili mbinu kwenye kipindi cha pili lakini wao wakaendelea na mfumo wao"
"Lakini kwao tunaweza kupata matokeo kwa kuwa watafunguka kujaribu kusaka ushindi."
Yanga itasafiri kwenda Ushelisheli kucheza mchezo wa marudiano kati tarehe 22-24, Feb 2018.
Katika hatua nyingine, Nsajigwa aligoma kuzungumzia tukio la mshambuliaji Obrey Chirwa kukosa mkwaju muhimu wa penati.
Mmoja wa waandishi wa habari alitaka ufafanuzi juu ya Chirwa kuachiwa majukumu ya kupiga penati licha ya kutokuwa na rekodi nzuri,
"Na wewe nakuuliza kwani kafunga mara ngapi?," Nsajigwa alimuhoji aliyeuliza swali.
Chirwa amekosa penati tatu kati ya penati tano alizopiga katika kipindi cha miezi miwili.

ADVERTISE HERE