Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema wameridhishwa na alama moja waliyopata katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc hapo jana licha ya kuwa walitamani kupata alama tatu
Hersi amesema wachezaji wa Yanga walionyesha ukomavu wakitokea nyuma mara mbili na kulazimisha sare ya mabao 2-2 katika mchezo mkali uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
"Tunawapongeza wachezaji wetu kwa kuonyesha ukomavu na kuweza kupata alama moja katika mchezo ambao walilazimika kupambana wakitokea nyuma mara mbili kusawazisha magoli. Azam Fc wana timu nzuri, wamefanya usajili mzuri nafikiri msimu huu watakuwa na timu imara sana"
"Kwa sasa focus yetu tunaielekeza kwenye michuano ya ligi ya mabingwa. Jumamosi tunakabiliwa na mchezo muhimu dhidi ya wapinzani wetu mabingwa wa Sudan Kusini. Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi uwanja wa Azam kutuunga mkono katika mchezo huu ili tuweze kupata matokeo mazuri"
"Jambo jema michezo yote miwili itachezwa hapa hapa Tanzania," alisema Hersi
Zalan Fc watachuana na Yanga katika mchezo huo ambao utapigwa Septmba 10 saa kumi jioni katika uwanja wa Azam Complex na mchezo wa marudiano kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Septemba 17