Kiu ya mashabiki wa Yanga ni kuona timu yao inafanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Msimu uliopita Wananchi walikuwa wanyonge kwenye michuano hiyo baada ya timu yao kuondoshwa kwenye hatua ya awali wakipoteza michezo yote miwili
Katika michuano ya msimu huu, Yanga imepata bahati ya aina yake mechi zote dhidi ya Zalan Fc ya Sudan Kusini zikipigwa Tanzania
Mpango mkakati wa Kocha Nasreddine Nabi na vijana wake ni kuona wanamaliza mchezo mapema tu siku ya Jumamosi ambapo mchezo wa kwanza utapigwa uwanja wa Azam Complex
Yanga watakuwa wageni jina tu kwani Jumamosi Wananchi wataujaza uwanja wa Azam Complex kuipa sapoti timu yao
ADVERTISE HERE