Kamati ya Sheria na hadhi za Wachezaji inakutana leo Ijumaa kujadili mashauri yaliyowasilishwa kwenye kamati yao sakata la Tuisila Kisinda wa Yanga likitajwa kuwemo.
Kisinda alisajiliwa na Yanga dakika za mwisho katika dirisha la usajili lililofungwa August 31 lakini Mamlaka za soka zimemuwekea ngumu wakidai Yanga haipaswi kumtumia kwa kuwa usajili wake utaifanya Yanga iwe na wachezaji 13 wa kigeni kinyume na kanuni ya 62 (1) ya ligi kuu toleo la 2022
Hata hivyo Yanga iliandika barua kwa Kamati hiyo kuomba Kisinda achukue nafasi ya Lazarus Kambole ambaye atakuwa nje kwa muda mrefu akisumbuliwa na majeruhi
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Said Soud amethibitisha Kamati yake kukutana akibainisha kuwa ni utaratibu wao kukutana mara baada ya usajili wote kukamilika ili kupitia pingamizi zilizopo baada ya usajili.
"Hatuna kawaida kuzungumza mapingamizi kabla ya kupitia lakini kikao kipo na tutajadili masuala ya usajili wala sio mambo ya madai hivyo suala la Kisinda na Joash Onyango linahusiana usajili litafanyiwa kazi," alisema