Wananchi wameanza vyema msimu wa ligi ya mabingwa wakiifumua Zalan Fc mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Ni matokeo ambayo kila shabiki wa Yanga alikuwa akiyasubiri na kwa hakika ingekuwa kalamu kubwa ya mabao kama washambuliaji wa Yanga wangekuwa makini
Fiston Mayele amefunga mabao matatu 'hat-trik' huku bao jingine moja likikataliwa na mshika kibendera
Feisal Salum 'Fei Toto' alifunga bao moja na pia akitengeneza bao moja
Yanga imemaliza nusu ya kazi, bado nusu nyingine itahitimishwa Septemba 17 hapo katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Hivi ndivyo unapaswa kuanza michuano mikubwa barani Afrika..!



ADVERTISE HERE