Baada ya kufunga hat-trik katika mchezo wa mkondo wa kwanza ligi ya mabingwa barani Afrika, mshambuliaji Fiston Mayele ndiye mchezaji anayeogopwa zaidi ya Zalan Fc kuelekea mchezo wa marudiano hapo kesho
Kocha Mkuu wa Zalan Fc Mawein Deng amekiri kuwa Mayele na kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' ndio wachezaji wanaomnyima usingizi
Hata hivyo Deng amesema kikosi chake kimekuja kupambana hivyo Yanga wasitarajie mchezo mwepesi
"Tunatarajia mchezo mzuri na wa ushindani tumejiandaa kushindana lolote linaweza kutokea"
"Yanga ni timu kubwa inawachezaji wengi wazuri lakini tunahofia zaidi mchezaji aliyevaa jezi namba 9 (Mayele) na yule namba 6 (Fei Toto)"
"Tumekuja kupambana tutapambana hadi dakika ya mwisho bado tuna nafasi ya kufanya kitu dakika 90 ndio zitaamua nani anatakiwa kuendelea hatua inayofuata," alisema