Kwa Mayele watalia wengi msimu huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Sep 2022
Kwa Mayele watalia wengi msimu huu

Mshambuliaji Fiston Mayele ndio habari ya mjini kwa sasa akiendeleza kasi ya kupachika mabao aliyoanza nayo msimu huu

Jana Mayele alifikia rekodi iliyowahi kuwekwa na Mrisho Ngasa mwaka 2014 akifunga hat-trik mbili katika mechi za mtoani ligi ya mabingwa dhidi ya timu moja

Ngasa aliwapiga Komorozani mabao sita nae Mayele akawapiga Zalan Fc mabao sita

Katika michezo saba iliyopita Mayele ameweka kambani mabao 11. Mchezo pekee ambao hakutetema msimu huu ni dhidi ya Azam Fc

Aliwafunga Simba mabao mawili katika mchezo wa Ngao ya Jamii, akafunga bao moja katika kila mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania, Coastal Union na Mtibwa Sugar

Kwa hakika huu unaweza kuwa msimu bora sana kwa Mayele kutokana na kasi aliyoanza nayo

Ni habari mbaya kwa timu zinazokutana na Yanga kwani wanaangukia mikononi mwa Mayele mwenye kiu ya kutetema katika kila mchezo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
44m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’