Mwananchi epuka propaganda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Sep 2022
Mwananchi epuka propaganda

Hivi karibuni kumeibuka mjadala usiokuwa na afya kwa klabu ya Yanga kuhusu nafasi ya Afisa habari wa klabu.

Kwanza sijui hoja hii imetoka wapi na kwasababu gani. Aliyeanzisha sijui alikuwa na lengo gani. Kila mmoja anapaswa kujua kuwa Yanga ni taasisi kubwa sana katika nchi hii inayoendeshwa kwa weledi na uwazi wa hali ya juu.

Klabu ya Yanga ilishatoka katika mazoea na imefika katika taaluma na weledi katika uendeshaji.

Klabu ya Yanga imefika katika mabadiliko ya uendeshaji wa Kisasa kutoka ule wa zamani ila wanaoanzisha hizi propaganda wao wamegoma kubadilika kuenenda katika usasa ambao Yanga ipo.

Duniani kote kila kiongozi/uongozi mpya unapoingia madarakani huhakikisha wanaajiri/kuweka watu ambao wanaona/hisi watawasaidia kukamilisha malengo yao waliyojiwekea.

Hivyo propaganda za kuwachagulia viongozi watu wa kufanya nao kazi zinatoka wapi? Hao wanaopiga kelele wamehisi mtu wao waliyemtuma hawezikupata hiyo nafasi?

Kwanini walalamike sana? Walitegemea kupata nini? Wanaona malengo yao hayatatimia? Yanga ni taasisi yenye katiba, kanuni, falsafa na utamaduni wake ambao ni lazima vifuatwe kwa yeyote anayeajiriwa, unaweza kuwa na sifa za ziada ila hujatimiza matakwa hayo hapo juu huwezi kuajiriwa.

Walipandikiza mtu wao ili malengo yao yatimie? Yanga ni taasisi ambayo haipaswi kumuamini kila mtu anayeletwa kwa maelekezo ya watu.

Taasisi kwanza halafu mtu baadaye. HEKO VIONGOZI WA YANGA KAMA MLIGUNDUA HUYO MTU NA KUMUWEKA PEMBENI.

Yanga imeajiri kampuni/jopo la watu wenye weledi wa hali ya juu kufanya usaili na mambo mengine ya msingi kabla hawajapata mtu sahihi mwenye vigezo vya kuajiriwa.

Jopo hilo lina hadidu za rejea ambazo ni matakwa ya taasisi.Usaili umefanyika na matokeo bado hayajawekwa hadharani, wao wamejuaje kuwa mtu wao hajapita?

Wanajua kuwa hana vigezo ndio maana wameanza kupiga kelele ili waonewe huruma na Jamii?

Maswali ni mengi kuliko majibu. Ewe mwananchi, tulipotoka tunakumbuka, wanataka turudi huko waanze kutucheka?

Kwa pamoja tuseme hapana kwa maadui wa maendeleo yetu, kila siku wanapinga na kukosoa kila ambalo uongozi hufanya.

Tuwe macho tuamke tushikamane na tuseme inatosha, tuliowachagua tuliwaamini.

Imeandikwa na Mwenyekiti wa zamani Kamati ya Ufundi Yanga, Dominic Albinus

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’