Al Hilal hawatutishi - Mayele

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Sep 2022
Al Hilal hawatutishi - Mayele

Mshambuliaji kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga Fiston Mayele amesema hawana hofu yoyote kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal ambapo mkondo wa kwanza utapigwa uwanja wa Benjamini Mkapa, Oktoba 08 2022

Yanga iliwaondoa Zalan Fc katika hatua ya awali ya michuano hiyo kwa ushindi wa jumla wa mabao 9-0 na sasa wanahitaji kupata ushindi mwingine dhidi ya Al Hilal ili waweze kutinga hatua ya makundi

Mayele amesema ubora na uzoefu wa kikosi chao unawapa jeuri na kuamini wanaweza kupata ushindi dhidi ya Al Hilal na kuwa hawana hofu yoyote kuelekea mchezo huo

"Hatuna hofu yoyote kuelekea mchezo dhidi ya Al Hilal, tunao wachezaji kama Bangala (Yannick), Morrison (Bernard), Aziz Ki, Djuma Shabani na wengine wenye uzoefu wa michuano hii mikubwa. Mimi nilicheza nikiwa AS Vita mchezo wangu wa kwanza ulikuwa kule Algeria dhidi ya JS Kabylie na pia nikacheza dhidi ya Raja Casablanca (Morrocco) uwanja ukiwa umejaa"

"Tutapambana ili kuhakikisha tunapata ushindi hapa nyumbani na tukienda Sudan pia tutapambana ili kupata matokeo yatakayotupa nafasi ya kusonga mbele," alisema

Yanga tayari imeanza maandalizi kuelekea mchezo ambapo kabla ya mchezo huo watacheza mechi ya ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’