Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema winga Tuisila Kisinda yuko fit kutumika katika mchezo wowote wa ligi na Kimataifa
Yanga ilimsajili Kisinda August 31 wakitumia vyema dakika za lala salama za dirisha la usajili kwa kumnasa nyota huyo mwenye kasi ya kimbunga akitokea klabu ya RS Berkane
Kulikuwa na sintofahamu kuhusu uhakika wa Kisinda kuitumikia Yanga lakini jambo hilo lilipatiwa ufumbuzi na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, wakimuidhinisha kuitumikia Yanga baada ya Wananchi kukamilisha taratibu zote za usajili wake ikiwa ni pamoja na kupata ITC yake kwa wakati huku wakimuuza Lazarus Kambole nchini Uganda
Nabi amesema tangu aliposajiliwa na Yanga, Kisinda alikuwa akifanya mazoezi chini ya uangalizi maalum na sasa wamejiridhisha yuko tayari kuitumikia Yanga
"Tuisila tangu ametua nchini alikuwa na mazoezi maalum chini ya kocha wa viungo anautimamu wa mwili yupo fiti kucheza mechi yoyote iliyo mbele yetu suala la kumtumia au kutokumtumia itategemea na mpango wangu siku hiyo"
"Ni mchezaji wa Yanga amesajiliwa ili kuitumikia timu hivyo ni lazima atapangwa. muda ukifika ataonekana akiitumikia timu," alisema Nabi
Kisinda huenda akaanza kuonekana uwanjani Oktoba 03 kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting ambao ratiba inaonyesha utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Hata hivyo Ruvu Shooting ambao ni wenyeji wa mchezo huo wamekuwa na kawaida ya kucheza mechi zao dhidi ya Yanga nje ya jiji la Dar es salaam