Ni wazi mshambuliaji Yacouba Songne amepona majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani miezi 10 sasa
Yacouba anashiriki program zote za mazoezi ya Yanga ikiwa ni ishara mwamba huyo yuko tayari kurejea uwanjani
Uongozi wa Yanga ulimpa muda zaidi wa kujiimarisha, hawakumjumuisha katika kikosi kinachoshiriki ligi kuu na michuano ya ligi ya mabingwa katika hatua hizi za awali
Yacouba anatarajiwa kurejeshwa 'kundini' kwenye usajili wa dirisha dogo, lakini itamaanisha kuna nafasi ya mtu ataichukua
Baada ya kuachana na Lazarus Kambole ambaye majeraha imekuwa changamoto kwake, Yanga imebaki na wachezaji 13 wa kigeni

ADVERTISE HERE