Wakati dirisha la usajili wa ligi kuu ya Vodacom likifunguliwa rasmi leo, wachezaji wa Simba Jonas Mkude na Ibrahim Ajib wameendelea kuwa gumzo mashabiki wakiwa na shauku ya kufahamu watachezea timu gani msimu ujao.
Licha ya wachezaji wote kukiri kufanya mazungumzo na timu yao Simba, lakini hakuna aliyesaini mkataba mpaka sasa.

Singida United na Yanga ndio zinazohusishwa na wachezaji hao kwa ukaribu ukiondoa klabu yao ya Simba.
Taarifa tulizozipata kutoka ndani ya uongozi wa Singida United ni kuwa kocha Hans van Pluijm ambaye amekwenda kwao Ghana kwa ajili ya mapumziko ameagiza wachezaji hao wapatikane.
Mkude alishaweka mezani dau lake la usajili kuwa ni Mil 70 na kuzialika timu zote zinazotaka kumsajili ikiwemo Yanga.
Ajib pia anadaiwa kufanya mazungumzo na klabu ya Yanga na Singida United pia lakini mpaka sasa bado hajafanya maamuzi ya wapi aelekee.

ADVERTISE HERE