Matchday : Ruvu Shooting vs Yanga, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Oct 2022
Matchday : Ruvu Shooting vs Yanga, NBC PL

Baada ya mapumziko ya wiki mbili kupisha kalenda ya FIFA, mabingwa wa nchi Yanga leo wanarejea 'mzigoni' katika ligi kuu ya NBC

Ni pale uwanja wa Benjamin Mkapa watakuwa wageni wa maafande wa Ruvu Shooting katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali

Inafahamika Oktoba 08 Wananchi wana jambo la nchi hapohapo kwa Mkapa katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal ya Sudan, mchezo wa leo utatumika kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo huo

Kocha Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi walifanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita dhidi ya Zalan Fc, leo mashabiki wa Yanga wanaweza kushuhudia mabadiliko makubwa katika safu ya ushambuliaji

Ruvu Shooting inayonolewa na Kocha Charles Boniface Mkwasa, msimu huu wako vizuri, wameshinda mechi tatu kati ya tano walizocheza kwenye ligi

Hivyo bila shaka watawapa Wananchi kipimo kizuri kuelekea mchezo wao wa ligi ya mabingwa siku ya Jumamosi

Yanga leo inatarajiwa kuwakosa baadhi ya wachezaji; Jesus Moloko, Chrispine Ngushi, Gael Bigirimana, Khalid Aucho, Bernard Morrison na Stephane Aziz Ki hawatarajiwi kuwa sehemu ya mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali

Hata hivyo kocha Nasreddine Nabi ana kikosi kipana, kukosekana kwa wachezaji hao haiwezi kuwa changamoto kubwa kwake

Mchezo utapigwa kuanzia saa 12:15 jioni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’