Mwananchiiiiiii, leo ndio Jumamosi, Oktoba 08! Tukuitane pale uwanja wa Benjamin Mkapa kumnyoa Mwarabu
Ndio! leo tunakwenda kumnyoa mwarabu mapema tu saa 10 jioni!
Hapa tunawazungumzia Al Hilal ambao watachuana na Yanga katika mchezo wa ligi ya mabingwa, mkondo wa kwanza
Yanga imejiandaa na mchezo huu kwa takribani wiki tatu, leo ndio siku ya kudhihirisha kuwa msimu huu Wananchi wana jambo lao Kimataifa
Kama huna tiketi hakikisha unatumia asubuhi hii kupata tiketi yako, bado tiketi za VIP C na Mzunguuko zinapatikana
Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga, mchezo wa kurejesha heshima ya Yanga Kimataifa
Leo ndio siku ya kuzima, kebehi na dharau kwa Wananchi katika michuano ya ligi ya mabingwa
Shamra shamra katika uwanja wa Benjamin Mkapa zitaanza mapema tu ili kuwavuruga waarabu kabla ya mchezo wenyewe
IWE JUA, IWE MVUA WATAPIGWA KAMA NGOMA.....!