Yanga imethibitisha kuwa safari ya Sudan itakuwa Jumamosi Oktoba 15 kwa usafiri wa ndege ya biashara (Ethiopia Air Line), ikitarajiwa kutua Sudan majira ya saa tano asubuhi
Ni siku moja kabla ya mchezo dhidi ya Al Hilal utakaopigwa siku ya Jumapili, Oktoba 16 saa mbili usiku
Msafara wa Yanga utakuwa na watu 51 ambapo Wachezaji ni 25, benchi la ufundi ni 11 na viongozi na mashabiki 15
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema tayari kuna maafisa wa timu hiyo wako Sudan kuweka mambo sawa ili kuhakikisha timu haipati changamoto yoyote nchini humo
Aidha yapo matumaini kuwa mchezo huo huenda ukarushwa mbashara na Azam TV baada ya majadiliano marefu kati ya Azam Media na Al Hilal
Taarifa kutoka Sudan imethibitisha kuwa Azam TV wamepewa haki ya kurusha mchezo huo mbashara. Hata hivyo bado Azam TV hawajathibitisha taarifa hiyo