Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amesema mfumo alioanza nao sasa kwa kuanza kuwapeleka wachezaji wake Gym ni katika jitihada za kuwaweka fit kuwaepusha na majeraha yasiyo ya lazima.
Aidha wachezaji wa Yanga kabla ya kuingia kambini walifanyiwa vipimo vya afya jambo ambalo lilikuwa halifanywi kabla yake.
Akizungumza baada ya kumaliza mazoezi jana Lwandamina alisema msimu uliopita wachezaji hawakuwa wameandaliwa vyema tangu mwanzo wa msimu hivyo kupelekea majeruhi ya mara kwa mara.
"Kabla ya kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mwanzo wa msimu vema wachezaji kufanya medical check-up kujua utimamu wao kiafya", amesema.
"Pia ni lazima waingie gym hii husaidia kupunguza majeruhi mara baada ya msimu kuanza, tuna ratiba ambayo kila mchezaji amepewa ambapo kuna muda huwa tunafanya mazoezi ya uwanjani kwa lengo la kutengeneza muunganiko wa wachezaji wapya tuliowasajili na kuufahamu mfumo ambao tutautumia kwenye mechi.
"Ni muhimu sana tukaboresha na kujenga mfumo bora wa matibabu ambao utapunguza lundo la majeruhi wa muda mrefu pia kuwajenga wachezaji katika saikolojia nzuri ya kucheza kwa moyo wote bila uoga wakijua kuna mfumo bora wa matibabu kikosini .
"Msimu uliopita nilisumbuliwa mno na lundo la majeruhi hivyo nisingependa kuona hali hiyo ikijirudia. Kila kitu kinaenda sawa ni imani yangu msimu ujao utakuwa wa mafanikio," amesema.
Yanga imeanza mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya Jumatatu iliyopita huku wiki yote ikitumika Gym.

ADVERTISE HERE