Keshokutwa Jumapili ni siku muhimu sana kwa Yanga pale watakapowakabili watani zao Simba katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Mchezo huu una umuhimu wa kipekee kwa sababu matokeo ya ushindi yatakuwa na athari chanya lakini matokeo tofauti yatakuwa na athari hasi
Yanga iwanahitaji mashabiki wake kwa wingi ili kuwaongezea hamasa wachezaji katika mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 11 jioni
Wananchi wametoka kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, wanahitaji kushinda ili kurejesha morali ya ushindi ya timu kuelekea mchezo utakaofuata kwenye ligi dhidi ya KMC kabla ya kuwakabili Club Africain katika mchezo wa kwanza wa mtoano kombe la Shirikisho ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 02
Morali ya wachezaji wa Yanga iko juu wakiwa na dhamira ya kushinda mchezo ili kuwapa furaha mashabiki waoΒ
Lakini pia matokeo ya ushindi yataishuhudia Yanga ikipanda kileleni mwa msimamo wa ligi na pengine kuanza kuweka sawa hesabu za kutetea ubingwa



