Asante sana Dickson Job

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Oct 2022
Asante sana Dickson Job

Sasa hivi zile kauli za sijui beki mfupi, sijui hawezi kucheza mechi kubwa hazisikiki tena

Ni kwa sababu wale mabeki wafupi pale Yanga wamewaziba midomo kwa vitendo baadhi ya wachambuzi ambao wanauzungumza mpira wa miguu kwa nadharia tu pasipo kuufahamu vyema

Alianza Kibwana Shomari akawashughulikia wale wachezaji wao wote ambao walikuwa wakiwaamini

Kwa sasa hakuna maswali tena Kibwana anapoonekana kwenye kikosi cha Yanga, maswali huibuka pale anapokosekana

Dickson Job nae amewanyamazisha wakosoaji kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya katika kikosi cha Yanga

Unaweza kuwauliza mashabiki wa Simba wasikupe jibu kuwa jana mshambuliaji Moses Phiri aligusa mpira mara ngapi?

Ukweli ni kwamba Job alimficha na kwa hakika alikuwa na kiwango bora sana katika mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Ni bahati mbaya tu kuna wachezaji kama Job ambao hawazungumzwi sana pale wanapofanya vizuri, wale wakosoaji wanasubiri wakosee ndio wazungumze

Hili linatokea kwa wachezaji wengi wa Yanga, ni vyema kusifia pale inapostahili ili uwe na uhalali wa kukosoa pale inapostahili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’