Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili watoza ushuru wa Kinondoni KMC katika mchezo utakaopigwa saa moja usiku
Matokeo ya ushindi kwa Yanga katika mchezo huo yatawashuhudia vijana wa Kocha Nasreddine Nabi wakipanda kileleni mwa msimamo wa ligi
Hata hivyo hautakuwa mchezo mwepesi kutokana na ushindani ambao KMC wanaonyesha kwenye ligi msimu
KMC inashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ikiwa imekusanya alama 13 katika mechi nane walizocheza
Katika mchezo uliopita waliichapa Azam Fc mabao 2-1 pia wakipata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba
Kwa Yanga ni mchezo muhimu kupata ushindi ili kurejesha morali ya ushindi baada ya kucheza mechi tatu pasipo kushinda
ADVERTISE HERE