Safari ya ubingwa imeanza sasa - Injinia Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Oct 2022
Safari ya ubingwa imeanza sasa - Injinia Hersi

Rais wa klabu ya Yanga Injinia Hersi Said amesema kesho katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold ambao utapigwa uwanja wa CCM Kirumba, ndio wataanza rasmi kampeni ya kutetea ubingwa waliotwaa msimu uliopita

Akizungumza leo Oktoba 28, 2022 jijini Mwanza katika mkutano na viongozi wa matawi Kanda ya Ziwa, Injinia Hersi alisema baada ya Simba kudondosha pointi jana, wanapaswa kuitumia vyema fursa hiyo kujiimarisha katika mbio za kuwania ubingwa

Injinia Hersi amewataka Wanachama na Mashabiki wa Yanga jijini Mwanza kuhakikisha timu inapata ushindi na kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi

Hersi amesema timu inapofasiri mikoani ni jukumu la Wanachama na Mashabiki wa mkoa husika kuhakikisha wanatoa sapoti inayohitaji ili kupata matokeo mazuri

"Tuhakikishe kesho tunakaa pale juu kwa tofauti ya pointi sita, biashara ni asubuhi na huu ni mwanzo tukusanye zetu mapema wameshaanza kuangusha bingwa anaanzia hapa kwenye hizi pointi tatu za kesho"

"Tumekuja hapa kutafuta pointi tatu, hakuna kitakachotupa faraja kama pointi tatu na hizi alama tatu ziko mikononi mwenu"

"Viongozi wa matawi, timu hii nimeikabidhi kwenu na sisi tutasikiliza maelekezo kutoka kwenu nyinyi ndiyo mnajua vitu gani vinahitajika ili tupate ushindi"

"Hii siyo Yanga ya Injinia (Hersi Said) ni Yanga ya wana Yanga, tukija hapa tunakuwa wasikilizaji tunaomba ushirikiano wenu kuleta matokeo kwenye timu yetu," alisema Hersi

Nae Mwenyekiti wa Yanga tawi la Mwanza Mjini, Salehe Akida alimhakikishia Injinia Hersi kuwa asiwe na wasiwasi kwani Mwanza haijawahi kuwaangusha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’