FT : Geita Gold 0-1 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Oct 2022
FT : Geita Gold 0-1 Yanga

Ushindi mwingine muhimu kwa Yanga mkoani Mwanza mbele ya Geita Gold ukiwafanya Wananchi waendelee kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi

Bao la mkwaju wa penati lililofungwa na Bernard Morrison kwenye dakika ya 45 lilitosha kuihakikishia Yanga ushindi muhimu

Yanga ilianza vyema mchezo huo ikifanya mashambulizi mfululizo langoni kwa Geita Gold katika dakika 20 za kwanza

Mashuti mawili ya Feisal Salum 'Fei Toto' yaligonga mwamba kabla ya Geita nao kuamka na kufanya mashambulizi langoni kwa Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kuondoka na alama zote tatu katika mchezo huo mgumu

Nabi amelalamika ratiba haikuwa rafiki kwani wamecheza mechi mfululizo na wanakabiliwa na mchezo mwingine wa kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain siku ya Jumatano

Baada ya ushindi huo, Yanga inarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Club Africain

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’