Yanga yapaa kwenda Shelisheli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Feb 2018
Yanga yapaa kwenda Shelisheli
Kikosi cha Yanga kimeondoka leo Jumapili asubuhi kwenda Shelisheli kwa ajili ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya St Louis.

Wachezaji 20 na viongozi 10 wamesafiri mapema leo tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kupigwa siku ya Jumatano, February 21.

Yanga imekwenda Shelisheli ikiwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo wa marudiano Yanga inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote. Hata ikipoteza kwa tofauti ya bao moja itasonga mbele ilimradi tu iwe imefunga bao ugenini.

Yanga imesafiri bila ya kinara wake wa mabao Obrey Chirwa anayesumbuliwa na maumivu ya misuli.

Wengine waliokosekana kwenye msafara huo ni Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Abdallah Shaibu, Yhana Nkomola na Donald Ngoma ambao ni majeruhi.

Pia wamo Andrew Vicenct Chikupe na Maka Edward.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
54m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’